Umejaza filamu na nyimbo kibao katika diski yako, labda ni magemu pia. Tamthilia je? Inaweza ikawa moja ya vitu hivi au ni mambo mengine kibao yamejaa kwenye kompyuta yako kiasi ya kwamba inakuwa ni vigumu ata pa kujua mafaili makubwa ya kufuta ni yapi hasa.
Unaangalia kompyuta yako na inakuambia diski C yako inakaribia kujaa
kabisa na hivyo unatakiwa ufute baadhi ya mafaili, ila ndio hivyo tena
kutokana na jinsi yalivyomengi hufahamu mafaili yapi ni makubwa au yapo
wapi hayo makubwa kutokana na wewe kuwa na mafolda mengi kwelikweli. Leo
tunakutambulisha kwa programu moja ya bure kwa watumiaji wa
kompyuta/laptop za Windows, inaitwa WinDirStat.
Ndio kuna njia zingine za kupunguza nafasi katika diski yako kama vile
kutumia programu wa Windows ifahamikayo kama ‘Disk Cleaner’, ila hiyo
haikuoneshi mafaili yako mwenyewe. Yenyewe inasaidia mafaili ya system
ya kompyuta tuu.
Programu ya WinDirStat inakupa uwezo wa kufahamu mafaili gani ni makubwa
na ni kwa ukubwa gani na pia inakupa uwezo wa kuyafuta kwenda kwenye
‘Recycle Bin’ au kuyafuta moja kwa moja kabisa bila kupitia Recycle Bin.
Unaweza kushusha WinDirStat bure kabisa hapa -> http://www.fosshub.com/WinDirStat.html
lets us You have great content I would like To thanks for this content
ReplyDeletehttp://www.softwarefunda.com/
There are many ways to reset a hard disk. After hard disk reset, we can get disk with initialized settings. We need to know the difference between low level format and normal format. In order to erase the disk and make the data unrecoverable, we need to use a low-level format. Here is an introduction to the low-level format and related knowledge. Hope it helps you solve the problem.
ReplyDeletehttps://www.reneelab.com/low-level-format-hard-drive.html